https://youtu.be/yTIcGY6mhm4
Nimefurahi sana kuona kuwa Rais wa Tanzania Dr. Magufuli anasema atawataja hadharani “majipu” yote yanayo takiwa kutumbuliwa. Kwakweli hata mimi nakubaliana naye kwani ni haki ya Mtanzania kujua hawa watu walioifikisha inchi yetu hapa! Hawa ni watu walikula na kutanua kwa pesa za wanyonge bila huruma yoyote! Sasa kwanini waonewe huruma eti wasitajwe hadharani?! Kisa! Mbona walitanua mbele ya macho yetu mchana kweupe?! #WatajweHadharani
Hivi karibuni nilikuwa na chat na mdogo wangu kuhusu mtu fulani ambaye juzi juzi amewekwa gerezani (ni jipu lile la bank ya $6m). Nilisema almost the same thing ambacho Dr. Magufuli amesema! Soma ? Kwakweli hawa mafisadi walifanya hata wale watu wanao tafuta pesa zao kihalali waonekane nao ni mafisadi. Tena hawa mafisadi wa TRA ndo sitaki hata kuwasikia waliona kama wao ndio wana hati miliki ya Tanzania! Viburi, dharau, na majivuno yasiyo semeka!! #WatajweHadharani maana hakuna namna!