Reposted from @farajanyalandu Najua kipindi hiki cha #COVID19 tunaweza kusahau uwezo wa binadamu kupambania jambo lake. Kwa sasa hivi tunapambana na hiki kirusi cha corona. Kimetukumbusha wasiwasi ndio maarifa bila kupepesa macho.Hapo nyuma niliwafurahia sana Prince Harry na Meghan wake. Waliamua jambo lao, waliamua watapendana. Mapenzi ni rahisi kuliko upendo. Upendo huwa ni parefu jamani. Lakini hawa wameweza kutuonyesha vyote: mapenzi na upendo. Lakini zaidi wametuonesha thamani ya hivyo vitu wawili. Upande mmoja namuonea huruma Harry na upande mwingine namuona ni shujaa, kati ya hawa wawili, yeye amesacrifice sana. Amejua kumtetea huyu dada. Haijalishi dada anastahili au hastahili. Watenda wema wa ukweli, hutenda wema kwasababu ni hulka yao na sio malipo kutokana na mtu wanayemtendea wema alivyo. Hata hivyo ametukumbusha uwezo wa binadamu kupambania jambo analolipenda, analoliamini na analotaka. AKIAMUA. Ukiona vinginevyo tofauti na unavyotarajia ujue ni maamuzi pia.
Tuendelee kupambana na corona. Tuendelee kutetea tunaowathamini na tunavyovithamini. GOD is still ON THE THRONE! #BeSafe – #regrann