Watoto na vipaji

Kama mmoja ya wazazi walio zaliwa na kukulia katika mazingira ya kiafrica ambapo wengi wazazi wengi miaka ya nyumba hawakuwapa watoto wao uhuru wa kukuza vipaji vyao. Wazazi wengi walikuwa na mtazamo yao ya ni nini wanataka watoto wao wawe wanafanya wanapo kuwa wakubwa.  Basi nami kwakweli nilijikuta nikiwa na mtazamo huo huo wakumnyima mwanangu uhuru wa kupata  full “exposure” ya vitu vile alivyokuwa akionyesha kuvipenda au niseme kuwa talented navyo kwani nilikuwa teyari nina picha ya ni nini mwanangu anatakiwa kufanya au kuwa.

IMG-20150415-WA0000
         …………….Babysister Blessing showing her talent.…….

Mwanangu ni anapenda sana basketball, mwanzoni nilimuacha ashiri mchezo huo alipokuwa elementary school. Alicheza mpaka darasa la saba lakini baadaye nilimzuia. Sababu haswa nilitaka a-constraint kwenye masomo zaidi kuliko michezo. Kitu ambacho kwa upande mmoja au mwingine hakikuwa kizuri kwani nili mnyima haki yake ya kuendeleza kile kitu ambacho roho uake inapenda sana.

Najua kuna wazazi wengi ambao bado wana mtazamo kama wangu, basi ngoja nikushauri kama utapenda. Ukiona mtoto wako anapenda kitu fulani au anaonyesha uwezo wa kitu fulani basi usidharau au kukatisha tamaa unless iwe ni kitu ambacho si kizuri kama kudokoa n.k  Usiweke nguvu myingi (pressure) kumuhiza akazanie no-no! Ila muonyeshe kuwa unam-support  kile anacho kifanya. Nasema usitumie nguvu sana kwani kama ni kipaji chake basi utazidi kuiona, na kama ni kitu cha mpito tuu basi baada ya muda atapoteza interest ya hicho kitu.

Dunia ya leo ni vizuri mtoto akiwa malt-talented. Dunia ya sasa si kama ile ya wazazi wetu ambapo kama mtu ni Manager wa kapuni basi utakuta ana kuwa na ma secretary wawili, leo hii wanataka Manager ambaye ajua kutype na basic computer skills kwa kwasababu ya mambo ya confidentiality makampuni mengi wanapenda Managers wa type na kuhifadhi baru wenyewe ili kupunguza risk za kuvuja kwa siri za kampuni.

Ok. Nawatakieni malezi mema  🙂  🙂

Leave a Reply