Kwa masikitiko makubwa naomba niseme yangu ya moyoni. Kwakweli inasikitisha sana kuona baadhi ya watu situu wamekosa kustaharabika bali pia wamepungukiwa na ubinadamu kiasi cha kuhuzunisha sana. Hivi jamani kwanini hatuwezi kuheshimu watu haswa katika maswala ya “privacy”? Kwanini tunawavunjia watu heshima hata pale ambapo hawawezi kujitetea au kuzungumza nasi kueleza hisia zao? Imekuwa nitabia ya Watanzania kuweka picha za watu ambao wamefikwa na mauti kwenye mitandao bila kujali ni jinsi gani familia zao, ndugu, na marafiki watajisikiaje watakapo ziona hizo picha.
Matukio kama haya tumeyaona mengi lakini leo naomba niongelee hili la Mtanzania mwenzetu marehemu Alphonce Mawazo. Ambaye alikuwa mwanachama wa Chadema huko Geita kama sijakosea. Watu wameweka picha zake ambazo zinaonyesha jjnsi alivyo uliwa bila hata kuficha sehemu ya sura yake? Huko wapi ubinadamu wetu enyi taifa la Nyerere!! Ni technology ni ndiyo imetufanya tukose ubinadamu kiasi hichi?! Hivi mnajua kuwa hao marehemu wana ndugu zao? Wana watoto na wake /waume zao ambao wasingependa kuona ndugu zao wana dhalilishwa kiasi hichi?! Mfano mmoja wapo ni jinsi Joyce Kiria alivyo weka picha za marehemu kwenye IG bila hata huruma wala woga wowote hajaficha wala kuomba radhi watu kwa kuweka hizo picha. Nasio posti moja, hapana! Katika posti zote mbili zenye picha tofauti wala hajali kuwa kitendo hicho si kizuri kabisa! (Picha hizo za juu ni mimi ndio nimefunika sura ya marehemu Alphonce Mawazo, lakini Joyce Kiria kaweka kama zilivyo pigwa huko eneo la tukio).
Saa nyingine unakuta mtu kaweka picha ya mtu ambaye yupo kwenye geneza bila hata kuficha sura ya marehemu!! Au mtu mgonjwa hospitali bila kupata idhini yake! Kwamfano, juzi tumeona tukio la Rais kutembelea hospital ya Muhimbili. Ndio ni jambo jema, lakini nani aliwapa vibaya vya kuknyesha sura za wagonjwa kwenye media? Kwanini hawakufunika sura zao? Je mnajua mnakiuka haki za msingi za wagonjwa? Mnafikiri familia zao zilijisiaje kuona ndugu zao walio taabani sura zao zikisambazwa kwenye mitandao na Tv? Je unafikiri yule mgonjwa pale siku akiona zile video atajisikiaje? Au kwasababu uwezo wao wa kifedha ni mdogo ndio maana hakuna anayejitambua na kujali haki zao? Wengine ndiyo utakuta wanatumia picha za marehemu kutasaka umaharufu na “kiki” za social media!! Jamani!! SMHH!!
Watanzania wenzangu embu weka ubinadamu mbele kabla ya yote. Mambo kama haya ndio maana wenzetu huwa wanatoka kadri za watu wanaopaswa kuhudhuria ibada za maisha ya ndugu zao au hata kusema nani anaweza kutembelea hospitali pale anapokuwa anaumwa. Hizi tabia za kishetani na zakinyama inabidi tuziache wapendwa!Badilika!
Pumzika kwa amani ndugu Alphonce Mawazo. Ulichofanyiwa ni unyama wa hali ya juu. Walaaniwe wote walio shiriki katika kifo chako. Natumaini sheria utafuata na hatua kali zitachukuliwa! R.I.P!
Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa na watu wake.