Wema Sepetu katika ubora wake! Vazi limemkaa haswa aaa! Kapendeza sana! My dear Wema naomba leo nikushauri, unajuwa wewe ni our Sweetheart! Tunakupenda sana na kukutakia mema! Naomba usichukie kuhusu ushauri wangu kwani unatoka from a good place of my heart, na pia sio lazima uhufuate unaweza ukasoma na ukauwacha kama ulivyo! Na ninakuhakikishia bado nitakupenda bila kinyongo! …… Wema sikiliza: 《1》Hii karne ya 21 kuzaliwa mzuri tu haitoshi! Wewe ni mzuri sanaaaaaa! Lakini unamengi ya ku-prove ili umpate yule mume / partner unaye stahili kuwa naye KAMA KWELI HILO NI HITAJI LA MOYO WAKO!
《2》 Achana kabisa na watu /fans wako ambao saa zote wanakueweka katika muonekano wa “mashindano” na mtu fulani haswa Zari, wakati Zari got no time for nobody yani yupo busy na maisha yake! Wewe ishi maisha yako bila kupigizana kelele na mtu! Au kuweka mazingira fulani yanayo onyesha some sort of competition! Kumbuka mtu yeyote yule ambaye anataka kushindana na mtu jua huyo mtu teyari umesha mzidi ndio maana anataka aku-drug down to his /her level! Always choose “highway” na sio mashindano! 《3》Ngoja nikwambie ukweli, wewe na Zari wote ni wazuri sana tena to be fair labda niseme wewe umependelewa zaidi na figure kuliko Zari! Hata hivyo any man ambaye ni potential au well successful will absolutely pick Zari over you! Unajua kwa nini? Zari has proven herself kuwa (a) she knows what she wants in her life! And happiness is her number one priority! Na ndio maana aliamua kuachana na marehemu Ivan Ssemwanga na kuwa na Diamond! She prefers happyness over money (b) Zari has proven kuwa she can make her man to be the best of all! She did that twice! Kwa marehemu Ivan Ssemwanga na sasa kwa Diamond! Ndio, unaweza sema ulimpenda Diamond akiwa bado “Nasib Abdul” but mdogo wangu, wenyewe wanasema hivi “a man with dreams need a woman with vision”! Na hapo ndipo Zari alipokupiga bao! You knew Nasib’s dreams but you didn’t have VISION to take Diamond where he needs to be! Plus badala ya kuwa team player ukawa kama una compete na Diamond; kumbuka zile kauli kuwa “anatembelea nyota yako” toka kwa mashabiki wako na watu wako wakaribu! Zari aliacha yote kumjenga Diamond at least for the first two yrs ya relationship yao. Building Diamond ikamsaidia kujiendeleza na yeye pia kwa ku-expand her empire in Tanzania. Wakati alionekana kama amepoteza Dira ya maisha kwenye macho ya watu wenye mtazamo finyu lakini kwetu sisi wengine tulijua Zari is going to surprise them big time and she surely did! Kumbuka nimekwambia kuwa Zari nia yake ni kuwa na mwanaume ambaye will make her happy, and that is what exactly Diamond is doing! Spoiling her right before your eyes! Pia angalia Ivan Ssemwanga, pamoja na yote bado Zari alikuwa ndio Kimbilio na tegemeo lake! Kitu ambacho wewe mpaka dakika hii pamoja na kuteka people’s heart but none of them can trust you with their “treasure” or legacy! (c) Zari has proven kuwa she is not only a great partner but she can hold down a family as well! She’s strong, has good family values enough to make her own family kitu ambacho wanaume wengi waliofanikiwa wanapenda kuwa nacho! Na hapa siongelei kuwa na watoto kwani watoto ni mipango ya Mungu! Ninacho kisema hapa nikuwa “grounded” enough to make someone’s house a family friendly place ambapo mtu kama Dr. Mengi atakuwa excited, and proud enough kusema I’m going home na once in a while kuwaita some of his friends for dinner! Mpaka sasa kwa hili mdogo wangu Wema, umefeli kabisa! Siku zote waliokuzunguka mmh! only God knows who they are! Embu jifunze kitu kutoka kwa aunt Ezekiel! 《4》 My dear Wema, achana na kutafuta attention zisizo na kichwa wala miguu! Don’t let them losers and fools use you my dear! Kama kweli you want to have that potential man holding your hand then you need to prove kuwa you are a woman of character! Make your man feel secured kuwa hayupo kwenye “competition” with another man! Yani kuwa akija mwenye hela zaidi yake he’s out of the league! Hii inaweza ikawa ngumu kunielewa lakini mpaka utakapo elewa hichi ninacho kwambia basi tegemea kutumika na wanasiasa pamoja na wenye pesa za “mission-town” ambao wanatafuta kuandikwa kwenye magazeti ya udaku!
《5》 Kama nilivyo sema kuwa you’ve a lot tu-prove na kitu kingine ni kuonyesha kuwa you can stand strong alone na kua-achieve something for your own good! Kwamfano mimi sio such a “career woman” but I managed to get my college education. Nasio hivyo tu, nimelea mwanangu ambaye niko so proud of her! Plus, naishi mwenyewe hapa Marekani bila msaada wa mwanaume hivyo mwanaume yoyote yule atajua kuwa kama tumependana ni kwasababu zingine na mapenzi ya kweli nasio ugumu wa maisha wa hapa Marekani! Angalia, mfano wa karibu ni Jokate, she’s a great example kama utataka kujifunza kutoka kwake! You have to show some potentials!
《6》Lamwisho, achana na mashoga a.k.a “wadada wa mujini”! You have your sisters make them marafiki zako wa karibu. Unaweza ukawa na baadhi ya marafiki wazuri kwa kula “bata” but don’t let them be your close friends! Kwasababu naona wengi wao sio wazuri na mkikorofishana siri zako zote wanakutolea nje wakati wewe sioni kama unatabia ya kutoa siri za watu! Hivyo achana nao kabisa! Otherwise, mie nakupenda sana na nakutakia mafanikio mema. Najua bado unanafasi ya kufanya matengenezo! Kama nimekosea naomba unisamehe sana. ❤
Hii inaitwa Ukweli Mchungu, few can see the positive (and the bigger) part of it