Wapendwa wasomaji wangu natumaini baadhi yenu mtakuwa mmeona haya majibishano kati ya Wakenya na Watanzania kuhusuana na “Olduvai Gorge.” Chanzo cha majibishano hayo ni dada mmoja binti wa Raila Odinga aitwaye Rosemary ambaye ni muwakilishi wa vijana inchini Kenya. Rosemary alitowa speech UN mwaka jana wakati wa kongamano la “amani” na katika maelezo yake akasema kuwa Olduvai Gorge ipo Kenya kwamba hivyo ndivyo alivyo fundishwa shuleni (sikiliza video)
Sasa hii imewaudhi Watanzania nakusema kuwa anatakiwa aombe msamaha. Siku ya Juma Tatu kwa kupitia account zake za social media aliomba msamaha kama inavyosomeka ??
Labda niseme tu kuwa ukisoma “between the line” unagundua Rosemary wasn’t sincere kwa msamaha aliyo omba. Kuna some sort of ego!!………Mwana dada Sandra Mushi amekuwa kama “kinara” katika mdahalo huu baada ya kuandika barua ya wazi kwa Rosemary Odinga ambayo ilichapishwa na gazeti la Citizen (soma ??) Sasa mimi kwakweli vitu kama hivi vinaniwia vigumu kuongea sana kwani nina wanangu (watoto wa mdogo wangu Janeth) ambao baba yao ni Mkenya. Nisinge penda kutengeneza aina fulani ya chuki au kuwa questionable about my loyalty kwani family will always come first to me!! Hivyo nimewaachia wengine waendelee na huu mdahalo na zifuatavyo ni sehemu tuu ya mdahalo huo Ila swali ambalo sijapata jibu ni kuwa kama hii ilifanyika kwenye kongamano la UN inamaana Tanzania haikuwa na muwakilishi wake ambaye angepinga hiyo kauli wakati huo? Kwanini imechukuwa zaidi ya mwaka kuiona hili?!! Mimi nasema mchawi wa Watanzania ni Mtanzania mwenyewe!! Sisi wenyewe tumekalia kuabudu vya wazungu mpaka hata wazungu wenyewe wanatushangaa!! Watu wenye talent mnaamua kuwamaliza / kuwadidimiza kwasababu ya ubinafsi na chuki zisizokuwa na kichwa wala miguu!! Wazazi wangapi ambao huwa wanawapeleka watoto zao kwenye maeneo ya kihistoria na mbuga za wanyama kama sehemu ya kusherekea birtday zao kabla ya kufikiria kumfanyia mtoto party ambayo nyingi huwa na pombe na mambo mengine ambayo hayafai kwa watoto? Sasa mnalalamika nini Wakenya waki sema vyakwetu ni vyao?! Mbona nyinyi mnang’ang’ania vya wazungu!! Unakuta msanii anavaa Tshirt yenye bendera ya USA wakati yeye ni muwakilishi wa Tanzania na funny thing hata USA kwenyewe hajawahi kanyaga!! Sasa hiyo ni akili au tope!! Tujifunze kupenda vya kwetu, tutangaze vya uzuri wa inchi yetu!!……….hizi ni baadhi ya comments za watu
Okay! The question is, where is Olduvai Gorge at? Is that even a question!! Wake-up Watanzania it’s not too late!!