William Ernest Mjee Oucho: Ndoto yangu ya kua Engineer

William Ernest Mjee Oucho
Napenda nishee na nyie story ya safari yangu ya kutafuta kuwa muhandisi tangu nimekua na mpaka sasa nilipofika. Twende sambamba utajifunza kitu hapa.

Mwaka 1993, Jumatano moja ya tarehe 09 mwezi wa Sita, mama angu alinizaa na kunileta duniani, na kunibarikia jina la William, ambaye alikua ni marehem baba yangu mkubwa. Nikaishi na wazazi wangu wote baba na mama, kaka yangu (JUMA SELA), dada yangu (Zainabu), na mdogo wangu Benadetha(R.I.P) katika kijiji cha Utegi, wilaya ya RORYA (kama mnavyoniita), mkoani Mara.

Familia ilikua ya hali ya kawaida sana. Ilipofika mwaka 2000, nilijiunga na shule ya msingi Utegi, iliyopo kwa kukadiria ni kama Km 4 kutoka home. Nikasoma na kuhitimu 2007. Nilianza kuonekana kama taa, baada ya kuwa nafaulu vizuri katika masomo yangu, na kupelekea kujulikana kwa waalimu na baadhi ya watu. Mwaka 2003, nikapewa uongozi (Kiranja) kwenye darasa la watu (188). Nikawakilisha vyema shule yangu katika uandishi wa Insha uliohusisha wilaya nzima ambao uliuletea shule yangu ya Utegi sifa nzuri. Walimu walianza kuniona mbali tangu hapo na kuniombea sanaa ndoto zangu zitimie.

Ilipofika December 10, mwaka 2004, baba yangu alifariki nikiwa darasa la tano. Akatuacha na mama na familia ya baba mkubwa (Olambo Oucho) kama baba yetu mlezi! Tulisikitika na kuhuzunika sana ila tuliyasahau na kumuona baba yetu mkubwa kama baba yetu mzazi. Mwaka 2006, nilihitimu shule pale pale utegi Primary school. Chakushangaza ni kwamba hata kufaulu sikufaulu, mbali na kujitahidi sana darasani (sijui nini kilitokea), ila mwaka huo (awamu ya kwanza) walifaulu wanafunzi 12! Nilikasirika sana, nikasema nitarudia shule na nitafaulu kwa alama za juu sana. January 8, 2007 nikarudi shule kurudia darasa la saba nijaribu bahati yangu tena. Haikuchukua muda sana March 01, 2007 matokeo ya awamu ya pili yakatoka nikawa nimo kati ya watahiniwa waliofaulu kwa alama za chini 159/250? na kuchaguliwa kujiunga na shule ya sekondari PASTOR RAPHAEL ODUNGA, ilioko kijiji cha Buturi, umbali wa Km kama 18 kutoka nyumbani.

Sikua na namna nilitamani sana kusoma na wenzangu form One, nikamwambia mama yangu akatafuta njia kwa kushirikiana na baba mkubwa wakanihamishia NYANDUGA Secondary iliyoko kwenye Kata yetu. Jumatatu ya tarehe 07 March, nilianza shule nikiwa nimebeba jembe, ndoo ya maji, kwanja, rim paper (double A) na shilingi 26,000/= nikaanza masomo. Wiki iliyofuata Jumatatu ya tarehe 12/03/2007 tulianza mitihani ya mid-term test nikiwa na siku tano tuu shuleni, nilipata alama za kushangaza watu sanaa ndio ukawa mwanzo mzuri! Nilipenda sana Maths, Physics, Chemistry na Biology ndipo nikaona mimi naweza kuwa Engineer baadaye maana masomo hayo nayaweza vizuri.

Mbali na kwamba baba angu mkubwa alisomea uhandisi (Engineering) nlipomgusia kuhusu nia yangu mimi ya kusomaea fani hiyo pia alinitia moyo sana, na kuniambia nikazane kwani kuna chuo kipo Dar kinaitwa DAR TECH, wanachukua watu wanaopasua sana masomo kama hayo! Akanipa dondoo za raha ya chuo hicho; wanavyokula, chuo kipo katikati ya jiji la Dar, wanalipwa hela, hakuna kufanya usafi, ? basi nikaona huko ndo patanifaa, nikasema wacha nikomaeee na shule kwanzaa.

MAISHA YA NYANDUGA SEKONDARI:
Nilijitahidi sana kusoma na kukazania masomo ya sayansi nikijua nikimaliza naenda chuo cha Dar Tech. Baba mkubwa alituwekea hazina ya vitabu vya kujisomea, nikapambana hadi mwaka 2010 ilipo maliza form four hapo Nyanduga Secondary, matokeo yalitoka yakiwa mazuri kwangu, na kwa rafiki zangu wengine. Tuliofaulu na kuchaguliwa technical school tulikuwa watatu; David Kajode alipelekwa Arusha Tech, David Kimira alipelekwa Ubungo Maji na William Ernest Mjee Oucho.

Hutaamini, nilichaguliwa moja kwa moja kujiunga na CHUO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA Dar es salaam (Dar Tech), kusomea Shahada ya Uhandisi mitambo kwa miaka mitatu.????? ndoto ikawa imetimia kwa namna moja. Nilifurahi sanaa! Mama na kila mtu aliyejua walifurahia sanaa. Namshukuru hata Mbunge wangu wa jimbo (MH. LAMECK O. AIRO, Lakairo) aliniona kwa jicho lingine na kunitia moyo na kuniahidi kushikamana nami bega kwa bega mpaka nitakapofika.

SAFARI YA KUJA DAR:
Ilifika siku ya kutoka nyumbani kuanza safari ya kuja chuo, nikiwa mwenyewe kwa mara ya kwanza ? nilipofika tuu Tarime Km 14 kutoka home nikaibiwa pesa zangu zote, na nikarudi home tena kutafuta pesa nyingine. Nikapata pesa nikaanza safari kwa mara nyingine na kuja mpaka Dar. Nilipofika Dar nilipokelewa na mama mkubwa (Mrs. Cecilia Igogo), kisha kunipeleka nyumbani kupumzika. Kesho yake asubuhi mama alinisindikiza chuoni kufanya usajili na baadaye kuhamia chuoni kwani nilikua natakiwa nikae chuoni. Mama mkubwa ni mama mwema sana, alikua akipita kunisalimia na kuniombea kwa Mungu, alinambia niamini katika ninachofanya nitafanikiwa. Nilitii na nikamuahidi sitamuangusha. Nilisoma na hatimaye 2014, nikahitimu.

William na mama yake mzazi wakati wa sherehe za kumaliza chuo, Dar Tech

Ikawa furaha nyingine kubwa kwangu, kwa mama yangu, baba yangu mkubwa na kila mtu aliyetamani kuniona nafika hapo.
Nilitamani kuunganisha kuendelea kusoma ila kuna somo moja lilinifanya nisiweze kuunganisha, kwani matokeo yetu yalicheleweshwa kupelekwa NACTE, ikanibidi nikae mtaani kwa miaka miwili. Katika kipindi hicho cha miaka miwili nilitumia kupata uzoefu wa kile nilichosomea, ambapo baba yangu mkubwa (Mr. Otieno O. Igogo) aliniona na kunipeleka kiwanda kimoja cha kutegeneza juice cha (U-fresh food), Tegeta. Nilifanya kazi pale kama fundi mchundo wa mashine hizo. Baadaye milango ya kazi ilifunguka na kujiunga na moja ya kampuni kubwa hapa nchini ya Kuzalisha Umeme na Kusambaza gesi (Songas Power Plant), iliyopo Ubungo. Nilifanya kazi pale huku nikiwa najitegemea sasa, naishi kwenye chumba changu cha kupanga.

Ilipofika mwaka 2016, nikasema lazima nijiunge kumalizia masomo yangu ya Shahada ya kwanza. Nilifanikiwa kufanya hivyo, nikapata chuo kile kile, fani ile ile, na nikaanza masomo rasmi ya kuitwa Engineer. Nilianza masomo yangu ya shahada ya kwanza mwaka 2016, na nikadumu kwa miaka mitatu, hadi kufikia june 10, 2019 nilipohitimu rasmi na kuweza kufaulu na kupata nlichokua nakitafuta kwa muda mreeefu! New Mechanical Engineer in Town.

Changamoto kila mtu anazo ndio maana hata sijaziongelea hapa, msije mkadhani nilikua nasona kwa raha raha, weee! ???? Ila natumia fursa hii kwanza kumshukuru Mwenyezi Mungu wa Mbinguni, muumba wa Mbingu na nchi kwa upendo na uhai alionikirimia. Pia napenda kushukuru kila mmoja kwa nafasi yake alivyoshirikiana na mimi kuniwezesha mimi kuwa hapa. Wanadarasa wenzangu, kuanzia darasa la kwanza hadi chuo Kikuu, ?!

? Mama yangu mzazi kapambana sana na mimi, kuhakikisha sikati tamaa, hata kama Inakuja gharika gani.

?Baba yangu mkubwa, Kwa kunionyesha njia na kutupatia elimu hakika, aliweza kutupa vitabu na sasa tunaona raha yake.

?familia ya Mr &Mrs Otieno Olung’a Igogo, mbarikiwe mpaka shetani aje awaulize mmewezaje wezaje???

? Lameck O. Airo, Erasto Airo bro asanteni kwa kila kitu kwa kipindi chote nilivokuwapo skuli.?Mbogi yangu ya Rorya, Robhin Edson, Edina Ziporah, Kajode, Mary, Triza, Omara, Vicky, Triza Wuod nam, Emma Lucas, na wengineo wengi ambao sitamaliza kuwataja hapa tumeshikana vyema na tuendelee hivi hivi?

Niwakaribishe katika mahafali ya kuhitimu shahada yangu ya kwanza ya uhandisi Mitambo, tarehe 28/11/2019 katika viwanja vya chuo chetu, tufurahie kwa pamoja maana nikishinda nanyi mmeshinda…NB: wanaosoma au una mpango wa kusoma, tia bidii sanaa utafanikiwa tuu, Mungu ni mwema na ni wa kwetu sote.NAWAPENDA SANA WOTE. ? THE END?

Leave a Reply