“Mashujaa hawa hatuwasikii kabisa”-Zitto Kabwe

Mwanamke Shujaa wangu siku ya Wanawake Duniani nimemkuta Zahanati ya Dutwa Halmashauri ya Wilaya Bariadi nikiwa kwenye ziara ya Taasisi ya Benjamin Mkapa. Mama huyu ni Mhudumu wa Afya Mkuu (Medical Attendant). Anaitwa Amina Makaja. Ameajiriwa kama mhudumu wa Afya toka mwaka 1977. Katika utumishi wake amewahi kujikuta peke yake kwenye zahanati na kufanya kazi za Mganga, Nesi na Mhudumu. Ameokoa maisha kwa kutibu watu na kuzalisha kina mama wenzake. Hii ndio hali Halisi ya Sekta ya Afya Nchini. Ukosefu wa watumishi sekta ya Afya maeneo mengi vijijini husababisha kuwa mama wa aina hii wengi sana. Mashujaa hawa hatuwasikii kabisa. Lakini tunasikia malalamiko tu dhidi ya Manesi na wahudumu bila kujali ugumu wa kazi zao. Siku ya Wanawake Duniani itazame wanawake katika nyeti kama hizi. Mwanamke wangu wa Siku kama ya leo mwaka huu ni Mama Amina Makaja wa Zahanati ya DutwaFB_IMG_1457914757649-1Asante sana Mh. Zitto Kabwe kwa kuliona hilo! Mimi naamini mashujaa wakweli ndani ya Tanzania wapo vijijini lakini hawapewi nafasi ya kusikika kwenye jamii!! Lakini muda umefika na mabadiliko ya kweli yanakuja. Nani alijua mtu kama Dr. John Pombe Joseph Magufuli angeweza kuwa Rais wa Tanzania bila yakuwa na “connection” za kimjini?! Pamoja tunaweza!!………ubarikiwe sana mama shujaa

Leave a Reply