Ushindwe wewe mama unaebadili rangi ya kucha kila wiki lakini neti za watoto zimetoboka kubadilishi
Ushindwe wewe mama kila siku ukirudi nyumbani unawaza tamthilia zako wanao wanaogeshwa na kupikiwa na housegirl.
Ushindwe wewe mama unayepata muda wa kusogoa mtaani, unga wa lishe ya mwanao anakuandalia dada
Ushindwe wewe mama unayemtegemea mwalimu na housegirl wamfundishe mwanao kila kitu
Ushindwe wewe mama unaebadili pea za viatu kila siku wanao viatu wameshonashona mpaka fundi anashangaa
Ushindwe wewe mama usiyetaka watoto wako wachangamane na watoto wengine wala hutaki kumpa mtoto wa mwingine kitu chochote eti maisha magumu!
Ushindwe wewe mama usiyetenga muda kusafisha nyumba vizuri kila siku watoto vikohozi, mafua, upele eti unakimbilia hosp kwa specialist
Ushindwe wewe mama usiyetunza mazingira yako matakataka yamesambaa, mapampers ya mwnao yamesambazwa na kunguru mtaa mzima halafu unajiita mzuri
Ushindwe wewe mama mwenye mtoto mchanga mikucha kama mwewe! Mtoto unamuogoshaje? Halafu kutwa mi-perfume! Hujafundwa?
Happy mother’s day
Jiongeze???????? Nimekaa nikawakumbuka wale ambao wanahasira na mama zao jamani! Nawaombeni muwasamehe tu kwakuwa wao pia ni binadamu wanakosea. Yaani inauma ukikutana na mtu anayemchukia mamake huwa wanalia kwa uchungu wakikueleza walivyotendwa na mama zao. Poleni kumbukeni kusamehe 7 mara 70 mtabarikiwa ajabu
Happy Mother’s Day to my sister Penny Tenga and Mama Tenga. ❤❤❤