Hongera sana Faraja Nyalandu kwa maono mazuri ambayo yana faida kubwa sana siyo tu kwa taifa letu bali kwa dunia nzima. Sauti ya mtoto ni sauti ya dunia kwani kinacho tokea leo effects zitakuwa baraka au laana kwa watoto wa vizazi vyote. Maamuzi mabaya ya wazazi yanaleta maafa kwa watoto wa vizazi vyote. Nipale wazazi kama wewe wanapo amua kuweka interest za watoto mbele ndipo wao. Ni mpaka pale wazazi wanapo acha kuwa selfish na kujali si tu watoto wao bali pia watoto wa wazazi wengine ndipo mabadiliko yanatokea. Hongera sana. Ulifanya maamuzi mema!…….Hongera sana kwa Getrude Clement nyota njema huonekana asubuhi!
G.C at UN -“As young people the future is ours but this is not the future we want for ourselves”! Ni jukumu la wazazi kuhakikishia watoto usalama wao katika nyanja zote za maisha, kijamii, na kimazingira. Huwezi kumwambia mtoto alale bila wasi wasi wakati anaomba nyumba ina tingishika. Lazima atakuwa na hofu! Mbaya zaidi na huzuni kubwa ni pale mtoto anapo muomba mzazi wake amuhakikishie usalama wa maisha yake wakati hilo ni jukumu lakwanza la mzazi! “You may think that we are too young to know about the risks and reality of climate change but we see that in our daily lives”-G.C Wazazi amkeni, badilikeni! #ItBeginsWithYou