@Regranned from @zamaradimketema – Ukiona MAAMUZI yako yanaangalia sana watu ujue una hatihati ya kuharibu maisha yako, kuna watu wanategemea sana ushauri na APPROVAL za ndugu, jamaa wa karibu na marafiki katika kila kitu bila kuchuja mengine aone ni ya kwake na yanamuhusu yeye tu, tusichofahamu linapokuja swala la hisia na mahusiano hakuna ubaya wa kusikiliza lakini fata kulingana na moyo wako, wengi wanaokushauri watakushauri kulingana na interest zao juu ya huyo mtu au vile wanavyomuona nje, lakini kumbuka wewe ndio unaishi nae na ndio mwenye moyo. Na zaidi kuna vingi unavyovijua ambavyo wao hata wawe karibu kiasi gani hawatakaa wavione, na hata kama mnahadithiana mara nyingi mnaongelea matukio na sio DETAILS, na kumbuka details ndio zinazotengeneza PACKAGE, na package ya ukweli unayoifahamu ni wewe, ila kwa kutaka kuridhisha watu unaweza jikuta unaacha kufanya maamuzi sahihi kwakuwa fulani kakwambia sio sawa tena kwa kuangalia tu kile ULICHOMUAMINISHA NACHO ama kumwambia, mwisho wa siku athari za UKWELI unabaki nazo wewe. Kumbuka tu Washauri ni wengi kwenye maisha lakini hawana msaada wowote na wewe pale linapokukuta, watu wapo kila siku lakini hupaswi kuwazingatia kiasi mpaka ukasahau lenye umuhimu na wewe kwa kuwapendezesha wao, wao wanafanya ya kwao bila kujali utawahukumu vipi na ya kwako yatakapoharibika utakaekaa ndani kulia ni wewe peke yako, na zaidi hawatakuwepo muda wote kwa ajili yako. – #regrann