Regrann from @zamaradimketema - PART 1
Wanawake kulegalega kwenye majukumu yao kunachangiwa sana na wanaume kuacha na kusahau WAJIBU wao ndani ya nyumba, lazima tuwe wakweli hivi vitu vinaenda pamoja
Kumekuwa na malalamiko mengi juu ya wanawake sikuhizi kuwa si watu wa kujali nyumba zao kama ilivyokuwa awali, na mzigo mkubwa wa lawama unatupiwa wanawake bila kuangalia kulia na kushoto kwenye MIANYA ya VYANZO vya namna hii
Katika majumba mengi sikuhizi ni ngumu kutofautisha nguvu ya mwanamke na mwanaume katika kile kinachowekwa mezani (kipato), zamani ilikuwa Baba ndio anaengaliwa kwa macho yote lakini sikuhizi wamama wamekuwa na mchango mkubwa sana kwenye familia nyingi, kitu ambacho ni kizuri na wote tunakubali, TUNACHOSAHAU kila Zuri linakuja na athari zake, tusifurahie tu mazuri halafu tukataka kufumbia macho NGUVU ZINAZOTUMIKA na JASHO LINALOTOKA katika kuleta mazuri hayo.
Hata vitabu vya MUNGU naamini vya pande zote vilizungumza juu ya MWANAMKE KUZAA KWA UCHUNGU na MWANAUME ATATAFUTA KWA JASHO. Lakini leo hii vitu ni tofauti, mwanamke haangaliwi kama mwanamke tena, na ndiomana hata waoaji wengi wa sikuhizi (sio wote) wanataka mwanamke atakaekuwa angalau na mchango kwenye familia, matokeo yake mwanamke anabeba misalaba yote na zaidi, atazaa kwa uchungu, atalea kwa mapenzi, na sio watoto tu hadi Baba, ataangalia na kulinda nyumba, na majukumu yote ya mwanamke yanayoonekana ni ya kwake, na pamoja na hayo yote BADO ATATAFUTA KWA JASHO, ambalo si jukumu lake, na kwa jinsi wanawake wa sikuhizi wanavyoweza kuchakarika hakuna ajabu ya kuona anachokileta nyumbani yeye ni kikubwa kuliko cha baba, kweli bila hata kufikiri mara mbili unaendelea kulaumu nwanamke wa namna hii kuwa labda hakai chini kumfulia mumewe n.k, hebu jiulize kuna MAJUKUMU MANGAPI yasiyo ya kwake anayojikuta ameyabeba!!
Na huenda yalistahili kufanywa na mwanaume, Kazi yake sio kutafuta kwa jasho lakini anatafuta, na huenda bila yeye kuhangaika watoto hawatasoma inavyostahili, mbali na hiyo bado atahangaika kuhakikisha kila kitu kiko sawa nyumbani hata anapokuwa mbali, hali ya kuwa Baba ni Baba tu na jukumu lake moja tena mara nyingine HALIFANYI INAVYOTAKIWA, maana wanaume wengine utakuta aki
Related