Sisi Binaadamu wengi ni watu tunaohofia MAWE, tunaishi katika hali ya kutafuta njia za kila aina za kukwepa kabisa kurushiwa na kuziba mianya yote itayoweza kutoa chakusema kwa adui zako kitu kinachopelekea kujikuta unaishi hadi maisha FAKE kwa kuhofia tu binaadamu, bila kufahamu mara nyingine ni vizuri kuyaacha yaje ili kujua yanatokea upande gani, yana sababu gani, yatakusaidia vipi na yatabadilisha nini pia kwenye maisha yako. Kwa upande wangu NIMECHAGUA kuyaokota na kujengea NYUMBA yangu, kila jiwe litakalorushwa kwangu nahakikisha siachi lipotee, nitaliokota na kuliongezea tu kwenye ujenzi wa nyumba yangu, hata kama lengo la mawe ni kuniumiza, nitahakikisha yananisaidia pia. Mawe ni BARAKA, mawe ni ongezo, na ni mafundisho pia. Tunajifunza mengi kupitia mawe yanayorushwa kwetu, tunakua zaidi, tunaimarika na kujijenga, tunafahamu nguvu tulizonazo na zaidi tunajifunza hata KUJIHADHARI Kupitia unavyonifikiria na kuyawaza juu yangu unafanya nijue nini natakiwa kufanya, unanifundisha wapi sitakiwi kuwepo nakadhalika, kiufupi UNANIAMSHA, na hata ule udhaifu unaohisi unaniumiza nao usichofahamu unanifundisha jinsi ya kuishi nao na zaidi kuufanyia kazi na kuufuta kabisa kama upo. Unaposema na kunisimanga juu ya jambo ni kunizindua juu ya jambo hilohilo hivyo kama lengo ni kukomoa unajikuta unafeli maana athari njema ulizoziacha utakuja kugundua ni nyingi kuliko zile mbaya ulizodhamiria.
Angalia kila jambo katika hali chanya na utaona faida yake, Usiangalie mawe kama SILAHA ukayakimbia ila badala yake yafanye ZANA katika kusimamisha himaya yako. MAWE yanasaidia KUJENGA!!