Zawadi si lazima pesa!

“We have been miseducated about gift-giving. We believe gifts must always bear a price tag or be given for a particular reason. The real joy in giving comes when we give what we have spontaneously, with no reason other than for the joy of giving.” Iyanla Vanzant  FB_IMG_1462969250894Watu wengi naona wanafikiria zawadi ni lazima iwe pesa au kitu fulani ambacho thamani yake inaweza onekana au kujulikana na watu wengi. Hayo mawazo yapo sana kwetu sisi ambao tunatoka Africa. Tunadhamini sana material things na kuonyesha umuhimu kidogo sana kwenye vitu ambavyo wengine hawawezi kuviona.

Zawadi ni kitu chochote kile mtu anakupa na inaweza ikawa katika mfumo wa pesa, vitu halisi, kukusaidia kimawazo, au kuchukua muda wake kwa ajili yako. Kwa mfano, nilisikiaga mtu anasema “yani amekuja kunisalimia mikono mitupu.”! Sasa unajiuliza hivi huyu mtu kaacha kazi zake na mambo yake kuja kuuona; wewe uwoni thamani ya muda wake, kama alipanda daladala inamaana alilipa nauli, na mambo yote ambayo ilibidi afanye au aache kufanya ili aje kukuona? Wenzetu wanasema “time is money”! kama mtu siyo mpenzi wako au ndugu yako wa karibu sana ambaye utakua free kumwambia akuletee zawadi basi hunabudi kushukuru mtu anapochukua muda wake kukujali kwani inaweza isiwe na thamani kwako wewe lakini kwake yeye is what all he / she has na akaamua ku-share na wewe!

Kikubwa katika utoaji  wa zawadi niitoke moyoni kwa dhati. Itafakari, je imetoka moyoni au ni mtu anatoa ili kukufurahisha wewe na wanao kuzunguka! Au mtu anakupa zawadi ili kuficha kitu fulani kwenye macho ya watu. Umeshaona yule mume anaye mjengea mke nyumba nzuri sana, anamnunulia gari la gharama kubwa, na kumvalisha nguo na mapambo ya thamani. Watu waliopo nje wakiona wanasema maisha si ndo yale, fulani anabahati sana. Kumbe laiti wangelijua kuwa humo ndani hakuliki, hakukaliki, wala hakulaliki!

Nachotaka kusema hapa ni kuwa, kama zawadi haitoki moyo kwa mtoaji basi hata kama utaipenda na kufurahiya kwa wakati huo mwishoni lazima utalipa gharama yake. Je unajua gharama utakayo lipa? Masimango, manyanyaso yasiyoisha, kila mtu atahitajika kujua kuwa yeye ndio aliyekupa, atataka amiliki maisha yako kwani alikupa zawadi bure, na mambo mengine kama hayo. Tujifunze kuthamini zawadi zote kwani zawadi si lazima iwe pesa!

Leave a Reply